Karibuni wapenzi wa mashairi katika toleo la pili la Diwani ya Tanzanet. Toleo hili linatolewa kwa kumbukumbu ya marehemu Hamidu R. Tambwe - ndugu yetu, malenga, mpenzi mwenzetu wa fani hii ya mashairi ambaye Mwenyeezi Mungu (Mwenye Kurehemu) alimchukua mapema mwezi wa Saba mwaka 2002. Tungo zilizomo katika toleo hili zote ni za kwake marehemu Tambwe ambaye aliziandika katika kipindi cha muda wa miaka kadhaa wa maisha yake. Ni matumaini ya Diwani ya Tanzanet kuwa wote mtaburudika na tungo hizi.
Kamati ya Wahariri,
DIWANI YA TANZANET.