"WANANET" ni jina la ukumbi wa mawasiliano ya e-mail ya Watanzania walio sehemu mbali mbali za dunia. Katika ukumbi huo, wajumbe hupashana habari zinazohusu Tanzania, hujadili mambo mbali mbali ya kijamii, kiuchumi na kisiasa yanayoihusu Tanzania na pia huelimishana juu ya mambo mbali mbali ya kiteknolojia na ufundi. 

Ukumbi huu wa WANANET ulianza rasmi mnamo tarehe 17 Julai 1992. Siku hizo za mwanzo waanzilishi wa ukumbi huu, Dr. Primus Mtenga na Dr. Mohamed Kaseko walikuwa wajumbe wa ukumbi wa Kenyanet. Katika ukumbi huo wa Kenyanet mambo mengi yaliyokuwa yanazungumziwa yalikuwa na uhusiano mdogo sana na Tanzania. Baada ya kutengeneza kwa ufanisi "mail alias", yaani anuani moja ya e-mail iliyowakilisha anuani kadhaa za e-mail za wanafunzi wake huko Florida A&M Univ/Florida State University, Dr. Primus Mtenga walishauriana na Dr. Mohamed Kaseko kuanzisha mpango kama huo kwa Watanzania. Katika mpango huo kila mjumbe alitakiwa kutengeneza "mail alias" ya wajumbe wote kwenye "account" yake ya kompyuta. Kila mjumbe alipaswa kuwa na orodha ya wajumbe wote ambayo ndio aliyoitumia kutengenezea alias. 

Kufuatana na taarifa zinazopatikana katika kumbukumbu za Dr. Mtenga, ukumbi huu ulipokuwa na umri wa wiki moja uanachama wake ulikuwa kama ifuatavyo:

Primus Mtenga 
Mohamed Kaseko 
Marion Kessy 
Conrad Shayo 
Jules Damji 
Mohamed Makame 
William Mbwambo 
Mrawira Massawe 

Siku za mwanzo ilikuwa shida sana kupata wafuasi. Ilibidi kutumia njia ya simu kushawishi na kubembeleza watu wajiunge na ukumbi huu. Kwa mfano Dr. Mtenga anakumbuka kumpigia simu mwalimu mmoja Mtanzania aliyekuwa sehemu za Atlanta kwa kutumia kizingizio cha kutafuta kitabu, kwani alikuwa amemsikia kwa jina tu. Baada ya mazungumzo kidogo ndipo alipomjuilisha kuwepo kwa ukumbi huu. Kwa bahati nzuri mwalimu huyo alijiunga na kuwakaribisha Watanzania wengine aliokuwa anawasiliana nao. Kwa kutumia njia hii mwisho wa mwezi wa Julai 1992 orodha ya wanaukumbi ilikuwa kama ifuatavyo: 


This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.                 Mtenga, Primus

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.             Kaseko, Mohamed

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.                 Kessy, Marion

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.                          Mbwambo, William

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.                Kalevela, Sylvester

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.             Shayo, Conrad

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.      Mrawira, Massawe

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.                 Damji, Jules

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.                   Makame, Mohamed

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.               Mshewa, Msafiri

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.                  Mushi, Selina

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.                Mussa, Renatus

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.                 Mrango, A.

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.                Kanduru, A.

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.                 Almasi, O.

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.                 Nkya, Estomih

Kundi lilipozidi kukua matatizo yalianza kujitokeza. Kwanza kabisa ilikuwa kama anuani yako haimo katika "alias" ya mtu anayetuma ujumbe wewe huwezi kupata huo ujumbe. Pili, sio kila mmoja alikuwa anaona rahisi kutengeneza alias kwenye account yake. Matatizo hayo yalitatuliwa na Bwana Renatus Mussa (This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.) aliyekubali kuwa mtu yeyote ambaye hawezi au hajui kutengeneza alias atume ujumbe kwake ili aweze kuurusha tena kwa wajumbe wote kutumia alias yake. Wanachama wengine wa mwanzo bado waliendelea kuwa na alias zao, lakini waliwasiliana mara kwa mara na Bwana Mussa kuhusu orodha mpya ya wajumbe. Kwa hiyo basi Bwana Mussa ndiye aliyekuwa mhudumu wetu wa kwanza wa ukumbi huu. 

Pamoja na kazi nzuri sana aliyoifanya Bwana Mussa, mbali na tatizo la kuwekwa anuani zote za wajumbe kwenye kila ujumbe uliotumwa, ujumbe uliotumwa na mjumbe kwenda kwenye anuani yake haukuweza kuwafikia wajumbe wote moja kwa moja. Bwana Mussa aliifanya kazi ya kutuma ujumbe kwa wajumbe wote kila alipopata nafasi, mara nyingi mwisho wa siku, hivyo kuwepo kuchelewa kidogo. Hapa chini ni mfano wa 'header' ya ujumbe uliotumwa kwenda kwa Bwana Mussa kisha yeye akautuma kwa wajumbe wote wakati ukumbi ukiwa na jumla ya wajumbe 50 kama inavyoonyesha. Angalia orodha ya anuani za wajumbe ambayo nayo pia ilikuwa inawekwa kwenye kila ujumbe! 


Date:         Fri, 12 Feb 93 22:24-0500

From:         This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Message-Id:   <This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.>

To:           This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              SMUSHI@UTOROISE, AMRANGO@UTOROISE, AKANDURU@UTOROISE,

              OALMASI@UTOROISE, This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., snyambo@utoroise,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.,

              This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.



From: xxxxxxxxxxxxxxxxx

To: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. (Renatus Mussa)

Date: Thu, 11 Feb 1993 17:44:34 +0000 (GMT)

Tatizo la anuani za wajumbe kutokea kwenye header ya kila ujumbe, pamoja na kuchelewa kwa ujumbe kuwafikia wajumbe wote lilitatuliwa na Dr. Willy Makundi, ambaye wakati huo alikuwa anafanya kazi huko Lawrence Berkeley Laboratories, Berkeley, California. Yeye, alijitolea kutengeneza alias kwenye mitambo yao ya UNIX. Alias hiyo aliipa jina WANANET. Anuani ya alias hiyo ikawa This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 

Katika mitambo inayotumia UNIX operating system, inawezekana kuweka kwenye /etc/aliases file, mstari wenye mfano: 

wananet: :include:pathname 

'pathname' ni file (with complete path) lenye orodha ya anuani za wajumbe ambao, ujumbe wowote utakaotumwa kwenda kwa wananet@system (hapa 'system' ni jina la system, kwa mfano huu, dante.lbl.gov) basi unasambazwa automatically, kwa wajumbe wote, mara tu unapopokelewa. File hilo lenye orodha linaweza kuwekwa kwenye account ya mtumiaji yeyote yule aliyepo katika hiyo mitambo, na yeye anaweza kuibadilisha orodha anavyotaka. 

Njia hiyo ndio aliyoitumia Dr. Makundi katika ile hatua ya kimapinduzi kabisa ya kurahisisha mawasiliano ya wajumbe wa ukumbi ambao ulianza kujuilikana rasmi kuwa WANANET. Hapo kabla, hapakuwa na jina rasmi la ukumbi, ila wengi walipenda kuuita TANZNET. Kuanzia hapo wajumbe wote wakawa wanatuma kila ujumbe kwenda This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. ambako ulisambazwa kwa wajumbe wote bila ya kuwekwa kwenye header anuani zote. Kila ujumbe ulionyesha To: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. ingawa uliwafikia wananet wote. 

Chini ya uhudumu wa Dr. Makundi, ukumbi ulikua kwa kasi sana kiasi cha idadi ya wajumbe kuzidi 100 kabla ya mwisho wa mwaka 1993. Ila haukupita muda, Dr. Makundi akatangaza nia yake ya kurudi Tanzania ifikapo April, 1994 hivyo akaomba mhudumu mwingine ajitolee kuchukua nafasi yake ya kuratibu shughuli za ukumbi wa WANANET. 

Wito wake uliitikiwa na Bwana Hashim Twaakyondo, aliyekuwa masomoni Tokyo, Japan. Kwa mujibu wa Bwana Twaakyondo, alitengeneza alias yake aliyoipa jina QWANANET kwa kutumia njia mbili tafauti kabla ya kutumia mbinu aliyoitumia Dr. Makundi. 

QWANANET ilianza kutoa huduma tarehe 7 Februari 1994 kwa kutumia anuani ya alias yenye jina (This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.). Mpaka kufikia mwishoni mwa Februari 1994, ilitumika mbinu ya kutumia .forward file. Yaani anuani zote za wajumbe ziliwekwa kwenye file lenye jina (.forward) lililowekwa kwenye 'home directory' ya account 'qwananet' katika mtambo (host) wa (susyor7.cs.shishu-u.ac.jp). Program inayoitwa 'sendmail' inayotumika kwenye UNIX operating system huwa inasambaza ujumbe kwenda kwenye anuani zote zilizoorodheshwa kwenye .forward file. Kwa namna hiyo, ndio QWANANET ilivyofanyakazi pale mwanzoni. 

Njia hiyo ilifanyakazi vizuri ila idadi ya wajumbe ilipoongezeka kukawa na ucheleweshwaji mkubwa wa barua zilizopitia huko na mara nyingine barua zilitumwa nakala mbili mbili. Hivyo Bwana Twaakyondo akaamua kutumia njia tafauti. Alitumia program ambayo ilifanyakazi ya kusambaza barua na akaiongezea mambo ili iwe inaangalia ni nani ametuma hiyo barua. Kama aliyetuma ni mjumbe basi barua yake ilisambazwa kwa wajumbe wote, la sivyo aliyeituma alipelekwa ujumbe wa kujuilishwa kuwa si mjumbe na barua yenyewe ilipelekwa kwake yeye (Bwana Twaakyondo) ili aamue kuisambaza au kuifuta. 

Njia hiyo ilitumika katika sehemu kubwa ya mwezi wa Machi 1994 ila nayo ikawa na matatizo makubwa. Kwanza ule ucheleweshwaji barua haukutatulika. Na pili, baadhi ya barua za wajumbe zilikataliwa pamoja na kuwa ni wajumbe sahihi wa ukumbi pale walipotumia anuani tafauti na zile zilizosajiliwa kwenye orodha ya Bwana Twaakyondo. Hapo ndipo alipoamua kutumia njia kama ile aliyoitumia Dr. Makundi. 

Njia hiyo ambayo inafanyakazi mpaka dakika hii inatumia mistari ifuatayo ambayo imewekwa kwenye /etc/aliases system file: 

# Mailing List 
qwananet: :include:/home/syori/syori/hashim/wananet/members 
qwananet-admin: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 

Kuweza kutengeneza alias kwa mbinu hiyo, inahitaji ruhusa ya mwenye kumiliki mitambo kwani katika system nyingi /etc/aliases file haliwezi kuongezwa kitu na mtumiaji wa kawaida. Na hata kama inawezekana, ni vyema kupata baraka za mwenye kumiliki mitambo au anayeiendesha (System Operator). Bwana Twaakyondo alipata ruhusa rasmi ya kufanya alias hiyo kutoka kwa supervisor wake. 

Kuanzia tarehe 7 Feb 1994 wajumbe ama walitumia anuani ya QWANANET (This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.) au anuani ya WANANET (This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.). Anuani zote mbili zilihudumia orodha sawa ya wajumbe ambao bado waliendelea kuitwa 'WANANET'. 

Wakati Dr. Makundi alipotangaza nia yake ya kurudi Tanzania, alikuwa amependekeza kuwa Dr. Primus Mtenga, iliyekuwa Florida State University, Tallahassee, ndio achukue nafasi yake kwa vile alidhani ingekuwa rahisi kwake, kwa vile ni mfanyakazi, kupata ruhusa ya mara moja ya kutengeneza alias kwa kutumia mbinu aliyoitumia yeye. Dr. Mtenga alikuwa tayari kuanzisha alias hiyo kwa kutumia anuani (This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.), ila majaribio ya mwanzoni yalileta matatizo makubwa ya kutumwa barua nyingi zisizo mpango kwa wajumbe wote, hivyo majaribio yakasimamishwa na alias hiyo ikasita kutoa huduma. 

Kuepuka hali ya kutoaminika ya nani achukue nafasi ya Bwana Twaakyondo, iwapo alias yake itaacha kufanya kazi kwa sababu yoyote ile, ilipendekezwa kuwa wajumbe zaidi wajitolee kutengeneza alias za akiba (backup aliases). Ilitarajiwa kuwa, alias mama (QWANANET), na alias za akiba zifanye kazi kwa wakati mmoja kama ni 'redundancy technique'. Mbinu hii pamoja na mambo mengine, ilitarajiwa: 

  • kuipunguzia kazi alias mama. 
  • kuzuia kukatika kabisa kwa mawasiliano ya 'WANANET' pindipo alias moja ikishindwa kutoa huduma kwa sababu yoyote ile ya mara moja au ya kudumu.

Mnamo 21 Machi 1994, Bwana Hassan Ali, aliyekuwa masomoni Chuo Kikuu cha Ottawa, Canada, akatangaza rasmi kuanzishwa alias ya akiba aliyoiita, OWANANET ('O' ikisimama kwa 'Ottawa'). Bwana Ali aliamua kuitumia moja ya anuani zake za e-mail, This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., kutumika kama alias ya akiba ya 'WANANET'. 

OWANANET ilifanyakazi kwa kuweka orodha ya anuani za wajumbe wote kwenye .forward file. Kwa namna hiyo alias ya akiba ya OWANANET ilifanyakazi bila ya matatizo yoyote makubwa. 

Alias ya OWANANET ilikumbwa na mikurubuko mingi hasa pale mwanzoni. Kwanza ilikuwa tatizo la 'stray mails'! Kwa kuwa hiyo ilikuwa ni anuani binafsi ya Bwana Ali, wako marafiki zake wachache ambao kimakosa, waliendelea kuitumia hiyo anuani kumtumia barua za kibinafsi. Matokeo yake barua hizo zilipelekwa kwa wajumbe wote. Mungu bariki, hazikuwa za siri!! Ukweli ni kwamba, ilikuwa ni kubahatisha hasa!! 

Baada ya kukomaa kidogo katika kutoa huduma, Bwana Ali akanuia kuondoa tatizo moja lililowafanya baadhi ya wananet kushindwa kuitumia alias ya OWANANET. Wananet hao wachache walipoitumia OWANANET barua zao zilishindwa kuwafikia baadhi ya wajumbe hasa wale wanaotumia VMS system. 

Bwana Ali akatangaza rasmi kufungwa kwa muda kwa mitambo ya OWANANET ili kushughulikia hilo tatizo. Kwa bahati mbaya, hatua za kurekebisha mambo, zilizaa tatizo kubwa zaidi lililosababisha kutumwa barua nyingi sana kwenda kwa wajumbe bila ya mpango. Hata hivyo, hali hii haikuchukua muda kurekebishwa.

Mwezi wa Mei, 1994, ndio akaanzisha utaratibu wa wajumbe kupata huduma kama ya kuondolewa kwenye orodha, au kumuingiza mjumbe mpya, au kubadilisha anuani au kurudisha anuani iliyoodolewa kwa muda, kwa njia ya automatic. Madhumuni makubwa, yalikuwa kurahisisha kazi ya kutoa huduma kwa wananet. Huduma za automatic zilifanywa kwa kutumia UNIX Shell pamoja na Awk programming. Huduma zenyewe zilipatikana kama inavyoelezwa hapa chini kutoka kwenye maelezo yaliyopatinaka automatically kutoka kwa Bwana Ali mjumbe anapotuma barua kwake yenye mada 'nipe maelezo': 


Hello Mjumbe, 

Hapa chini ni maelezo ya automatic services ambazo unaweza kuzipata kutoka kwenye mitambo yetu. Ombi lako lipeleke kwa kutumia anuani: 

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 

Ujumbe ukifika kwenye anuani hiyo unasambazwa kwa wadhamini wa alias zote. 

Anuani za alias zetu ni: 

  1. This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. mdhamini Hassan Ali 
  2. This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. mdhamini Hashim Twaakyondo 
  3. This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. mdhamini Joel Felix 

Anuani binafsi za wadhamini wetu kwa mpango huo hapo juu ni: 

  1. This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 
  2. This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 
  3. This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 

Tafauti na kuomba maelezo ambako ombi lako unaliweka kwenye "Subject" ya ujumbe wako, kuomba huduma zifuatazo ni lazima uandike maneno yatakayoelezwa hapa chini NDANI ya ujumbe wako. Kwenye Subject unaweza kuandika chochote na haiangaliwi kabisa. 

1. Kuondoa anuani yako kwenye orodha, tuma mail yenye mstari wa pekee wenye maneno: ondoa: anuani_yako 
Mfano: 

ondoa: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 

2. Kurudisha anuani yako baada ya kuondolewa kwa muda, tuma mail yenye mstari: rudisha: anuani_yako 
Mfano: 

rudisha: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 

3. Kumleta wavuni mjumbe mpya, mail yako iwe na mstari wa pekee wenye maneno: mjumbe: anuani_yake majina_yake Majina ya mjumbe sio lazima, na yasizidi matatu. 
Mfano: 

mjumbe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. Mr Hassan Ali 

4. Kubadilisha anuani yako, mail iwe na mstari wa pekee (ambao mara nyingi huwa mrefu sana, usijaribu kuukata) wenye maneno: badili: anuani_kongwe anuani_mpya 
Mfano: 

badili: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 

ANGALIA: 

i. Mbele ya maneno 'ondoa', 'rudisha', 'mjumbe', 'badili', ni lazima pawepo na colon ':' bila ya kuacha nafasi yoyote ile kati ya hayo maneno na hiyo colon. 

ii. Nyuma ya maneno hayo hapatakiwi kuwepo chochote, yaani mstari ni lazima uanze na hayo maneno. 

iii. Huwezi kuondoa anuani ambayo si yako. 

Tunakushukuru kwa kutumia huduma zetu za automatic. 

Mhudumu. 


Kwa bahati mbaya, huduma za automatic hazikuweza kupatikana kutoka kwenye alias nyingine za wananet zaidi ya OWANANET. Na zaidi, si wajumbe wote waliozitumia huduma hizo. Hata hivyo, ufanisi mkubwa ulipatikana kwa matumizi ya huduma hizo hasa kunusuru muda wa mhudumu wa OWANANET. 

Wito wa kutengeneza alias za akiba pia uliitikiwa na Bwana Odemari Mbuya, aliyekuwa masomoni, Chuo Kikuu cha Florida, Gainsville. Yeye alitumia mbinu tafauti kabisa kwenye VAX/VMS operating system, kutengeneza alias aliyoibatiza jina, NYAVU. Anuani ya alias hiyo ilikuwa (This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.). Alias hiyo ilianza kazi rasmi tarehe 25 Machi 1994 kama siku 4 tu tangu OWANANET iasisiwe. Hivyo, ilifika wakati, ukumbi wa wananet ukawa unazo alias nne za kutumika zote zikihudumia orodha sawa ya wajumbe. Alias hizi zilikuwa WANANET, QWANANET, OWANANET na NYAVU. 

Ilipofika April 1994, alias ya WANANET haikufungwa kama ilivyotazamiwa ila haikutoa huduma za moja kwa moja. Ilifanywa kwamba, kila ujumbe unaotumwa kwenda This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. upelekwe kwenda QWANANET kwa ajili ya kusambazwa kwa wananet wote. Hali imebaki kuwa hivyo mpaka wakati huu. 

Bwana Mbuya alibahatika kupata kazi iliyomfanya aondoke kutoka kwenye Chuo alichokuwa hivyo tarehe 9 Agosti 1994 aliifunga alias ya NYAVU. Kufungwa kwa alias ya NYAVU kukaitikiwa na Bwana Joel Felix aliyekuwa masomoni, Iowa State University, aliyetengeneza alias aliyoipa jina, TANZANET. Anuani ya alias hiyo ikawa, (This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.). Mbinu iliyotumika kutengenezea alias hiyo ni sawa kabisa na ile iliyotumiwa kutengenezea WANANET na QWANANET. Jina hilo alilolibuni Bwana Joel Felix (TANZANET) lilielekea kupendwa na wajumbe walio wengi, na kwa hiyo ikawa inatumiwa na wajumbe kwa wingi kutuma jumbe zao. TANZANET ilianza huduma za automatikali kwa kutumia programu inayoitwa "MAJORDOMO". Hii iliwasaidia wajumbe kujichukulia wenyewe mafaili kutoka This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. kama vile anuani za wajumbe na kadhalika. Alias ya This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. ilifungwa rasmi mwezi May 1997 baada ya Tanzanet kuanzisha huduma ya kulipiwa kwa kutumia mtambo wa PARRETT.NET na anuani ikajulikana kama This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Vilevile Bwana Joel Felix alianzisha na kuendelea kuhudia anuani ya viongozi wa Tanzanet aliyoiita This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. Hii anuani ilitumiwa kwa mawasiliano ya viongozi wa TANZANET pekee. 

Alias ya OWANANET ilifungwa rasmi tarehe 1 Machi 1995 kwa sababu na maelezo kama yafuatayo, aliyoyaeleza Bwana Ali alipotangaza rasmi kufungwa kwa alias hiyo: 


"Ukiamba vyako, na Mungu aamba vyake!" Nilidhani baada ya kuifanya mitambo kujiendesha yenyewe, mimi kazi ningekuwa sina tena! Kwa bahati mbaya, miezi kadhaa imekatika na bado wajumbe wamekuwa wakiendelea kuomba huduma kwa njia zisizokuwa za ki-automatic. Hii ni pamoja na kufanya jitihada kadhaa za kuwaelimisha wajumbe kama vile maelezo marefu yanayopelekwa kwa kila mjumbe mpya, huduma ya kupata maelezo automatically kutoka kwangu, na maelezo mengine kadhaa niliyoyatoa kwenye ukumbi. 

Nilidhani itatokezea siku, isiyo ya mbali, ambapo wajumbe karibu WOTE wangetumia huduma za ki-automatic. Siku hiyo sikuiona dalili ya kutokezea! Wakati siku zinasonga, na kazi iliyonileta ikikaribia mwishoni, muda nao umekuwa adimu kwangu. Katika hali iliyopo, siwezi tena kutoa huduma kama inavyotakikana. Sasa badala ya kujipiga kifua kujidanganya kuwa nitaimudu tu hiyo kazi, nimeona niwe mkweli, na nikubali kushindwa. Kwani asiyekubali kushindwa si mshindani. 

Ndio maana leo hii, nimeamua kutangaza rasmi kuwa ALIAS YETU YA OWANANET (This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.) IMEFUNGWA RASMI!..... 


Njia ya kutoa huduma ki-automatic haikupotea bure pale Bwana Ali alipoifunga mitambo ya OWANANET. Kwa kushirikiana na Bwana Ali, Bwana Twaakyondo aliweza kuifanya njia hiyo kuweza kupatikana kwenye mitambo ya QWANANET kuanzia tarehe 8 April 1995. 

Kufungwa kwa WANANET, NYAVU, na OWANANET, kumesababisha kubakia alias mbili tu zinazofanyakazi mpaka wakati wa kuandikwa historia hii. Alias zinazofanyakazi ni QWANANET na TANZANET kwa pamoja zikihudumia zaidi ya wajumbe 400 duniani kote. 

Zimewahi kufanywa jitihada mbali mbali za kuratibu majadiliano ya ukumbi huu ili yaweze kuwa ya manufaa kwa wajumbe na Watanzania wote kwa ujumla. Jitihada hizo kwa bahati mbaya hazikufanikiwa. Aidha wajumbe waliwahi kutoa wazo la kuchapishwa kigazeti (Newsletter) kitakachotoa muhtasari wa maongezi na mijadala ya WANANET. Kigazeti hicho kilikusudiwa wasomaji walioko Tanzania. Mawazo hayo nayo hayakufika popote. 

Ili kufanikisha suala la kupatikana habari kutoka Tanzania ilipendekezwa kuwa wajumbe watoe kiingilio cha US$10. Upokeaji wa viingilio hivyo umefanywa na hatua za kutafuta njia nzuri na ya kuaminika ya kupatia habari za Tanzania zimo mbioni wakati wa kuandikwa historia hii. 

Moja kati ya mafanikio makubwa ya ukumbi huu ni kuanzishwa kwa mchango uliopendekezwa na Dr. Willy Makundi wa kuweza kuwasaidia watafiti na wafanyakazi wengine walioko Tanzania waweze kumudu kulipia gharama za kutuma na kupokea e-mail wanapoitumia njia hiyo kuwasiliana na nje ya nchi kwa masuala ya kazi zao. Mchango huo wa hiari bado unaendelea na katika hatua za mwanzo, chini ya usimamizi wa Bwana Rama Mwikalo, Bwana Hassan Ali, Bwana Odemari Mbuya, na Dr. Willy Makundi, ilianzishwa node ya e-mail, Kimandolu, Arusha. Node nyingine imo mbioni kuanzishwa Dar es Salaam wakati wa kuandikwa historia hii. Node ya Dar es Salaam ambayo ilitazamiwa kuwa IFM, imecheleweshwa na urasimu uliotokana na masharti ya "warranty" ya kompyuta mpya zilizowekwa hapo IFM. 

Watu mashuhuri waliopata kuwa wajumbe wa ukumbi wa WANANET ni pamoja na Prof. Issa Shivji, Prof. Haroub Othman, Dr. Walid Kabouru, wote wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 

Mwezi wa Julai, 1995 ilianzishwa rasmi Bodi ya WANANET na wajumbe wafuatao walichaguliwa kushika nafasi mbali mbali: 

Mwenyekiti - Dr. Primus Mtenga 
Katibu Mtendaji - Bw. Sabinus Komba 
Naibu Katibu Mtendaji - Bw. Hassan Ali 
Mshika Fedha - Bw. Rama Mwikalo 
Wajumbe: 

Dr. Joseph Mbele 
Bw. Joshua Ndege 
Bw. Hashim Twaakyondo 
Bw. Joel Felix 
Bw. C. Mwasambili 
Bw. Edmond Lyatuu 
Bw. Michael Wambali 
Bi. Mary Likwelile 
Bw. Mohammed Seif 

Toleo la kwanza limetayarishwa na: 
 

Hassan Ali 
Primus Akwanza Mtenga 
Hashim Twaakyondo 
Joseph Mbele 
Mohammed Kaseko 
Mei 4, 1995. 

Imesahihishwa na kuongezewa maelezo na: 

Hassan Ali 
Oktoba 9, 1995.